TAHADHARI YA ONGEZEKO KUBWA LA WINGI WA MAJI KATIKA MITO KUNZIA TAREHE 07 APRILI HADI APRILI 14, 2026

Taarifa va utabiri wa mafuriko unaonesha Kuna uwezekano wa ongezeko la wastani na Juu va wastani la wingi wa maji katika baadhi ya mito ambalo linaweza kupelekea mafuriko katika kipindi cha kuanzia tarehe 07 Aprili hadi 14 Aprili 2026
Kwa mujibu wa utabiri umebainisha baadhi ya maeneo yanayotarajiwa kukumbwa na mafuriko ambayo ni Kijiji cha Ving'awe, Zombo Tindiga, Daraja la Mkundi, Dumila, Gongo la Mboto, Mkata,Miyombo, Munisigara, Masanze, Kibaoni, Malui, Handeni- Turiani Road, Zombo, Vingunguti Bridge,Misufini-Kilosa, Ruvu - Moro Road Bridge, Magomeni-Kilosa, Gulwe, Kilimanjaro, Kisala, Berega Darajani na Changalawe Kilosa, hivyo Bodi inatoa wito kwa wananchi wanaoishi katika maeneo hayo kuchukua tahadhari ili kujilinda na athari zinazoweza kujitokeza
Aidha mamlaka husika zinasisitizwa kuondoa vizuizi vya maji katika madaraja ili kuruhusu mtiririko sahihi wa maji na kupunguza hatari ya mafuriko mbali na hilo, Bodi itaendelea kufuatilia kwa karibu mwenendo wa viwango vya mitiririko ya maji na kutoa taarifa zaidi



