TAHADHARI YA ONGEZEKO KUBWA LA WINGI WA MAJI KATIKA MITO KUANZIA TAREHE 06 MEI HADI 13 MEI 2026.

Taarifa za utabiri wa Mafuriko zinaonesha uwezekano wa kuongezeka kwa wingi wa maji katika baadhi ya mito kwa kiwango cha wastani hadi juu ya wastani hali ambayo inaweza kusababisha Mafuriko katika kipindi cha kuanzia tarehe 06 Mei hadi 13 Mei 2026.
Kwa mujibu wa utabiri maeneo yanayotarajiwa kukumbwa na mafuriko ni: Kijiji cha, Zombo–Tindiga, Daraja la Mkundi, Dumila, Mkata, Miyombo, Masanze–Mkondoa, Masanze–Miyombo,, Zombo, Misufini–Kilosa, Kibaoni–Kilosa, Magomeni–Kilosa, Kilimanjaro–Turiani, Kinyasungwe–Kongwa, Kisala, na Changarawe–Kilosa.
Bodi inatoa wito kwa wananchi wanaoishi katika maeneo haya kuchukua tahadhari stahiki ili kujilinda dhidi ya athari zinazoweza kujitokeza.
Aidha mamlaka husika zinasisitizwa kuondoa vizuizi vya maji vilivyopo katika madaraja ili kuruhusu mtiririko sahihi wa maji na kupunguza hatari ya Mafuriko.
Bodi itaendelea kufuatilia kwa karibu mwenendo wa viwango vya mitiririko ya maji na kutoa taarifa zaidi kadri itakavyohitajika.




