Tahadhari ya Ongezeko Kubwa la Wingi wa Maji katika Mito kuanzia Tarehe 11 Machi hadi 16 Machi 2026.

Taarifa ya utabiri wa mafuriko inaonesha kuna uwezekano wa ongezeko la Wastani na Juu ya wastani; la wingi wa maji katika baadhi ya mito ambalo linaweza kupelekea mafuriko katika kipindi cha kuanzia tarehe 11 Mach hadi 16 Mach, 2026,
Aidha Kwa mujibu wa utabiri umebainisha baadhi ya maeneo yanayotarajiwa kukumbwa na mafuriko ambayo ni Kijiji cha Kibaoni, Malui, Tindiga, Magomeni-Kilosa, Kisala na Kijiji cha Kilimanjaro, Miyombo na Baadhi ya maeneo yaliyopo Bonde la Mto Msimbazi hivyo Bodi inatoa wito kwa wananchi wanaoishi katika maeneo hayo kuchukua tahadhari ili kujilinda na athari zinazoweza kujitokeza.
Aidha, mamlaka husika zinasisitizwa kuondoa vizuizi vya maji katika madaraja ili kuruhusu mtiririko sahihi wa maji na kupunguza hatari ya mafuriko.
Bodi itaendelea kufuatilia kwa karibu mwenendo wa viwango vya mitiririko ya maji na kutoa taarifa zaidi.
“Tone la maji lazima lihifadhiwe “



