WASOMA TAKWIMU WAPEWA MAFUNZO YA MATUMIZI YA MFUMO WA KUTUMA TAKWIMU KUPITIA SIMU JANJA

Bodi ya Maji Bonde la Wami/Ruvu leo imeendesha mafunzo kwa Wasoma Takwimu kuhusu matumizi ya mfumo wa kidijitali wa kutuma takwimu kupitia simu janja.
Mafunzo hayo yamewahusisha Wasoma Takwimu kutoka Dar es Salaam, Dodoma na Morogoro, wanaohusika na ukusanyaji na uwasilishaji wa takwimu kutoka vituo vya mvua, vituo vya kupima kina cha maji (Water Level) pamoja na visima.
Mafunzo hayo yamefanyika kwa baadhi ya vituo muhimu vya msingi (Primary Stations) vilivyo katika Bonde la Wami/Ruvu, ikiwa ni hatua ya kuimarisha upatikanaji wa takwimu sahihi, zenye ubora na kwa wakati.
Matumizi ya mfumo huo kupitia simu janja yanalenga kurahisisha na kuongeza ufanisi katika ukusanyaji na uwasilishaji wa takwimu, ambazo ni muhimu katika ufuatiliaji wa hali ya rasilimali za maji, upangaji na utoaji wa maamuzi katika usimamizi wa rasilimali za maj.
Mafunzo haya ni sehemu ya mwendelezo wa zoezi hilo, ambapo awamu inayofuata (Phase II) itahusisha Wasoma Takwimu kutoka vituo vingine ndani ya Bonde la Wami/Ruvu.
Bodi ya Maji Bonde la Wami/Ruvu — Takwimu sahihi, kwa wakati kwa usimamizi bora wa rasilimali za maji.
Tonelamajilazimalihifadhiwe



