Salamu za rambirambi

Mkurugenzi, Menejimenti na Watumishi wa Bodi ya Maji Bonde la Wami/Ruvu tunatoa pole za dhati kwa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, pamoja na familia yake kwa kuondokewa na mpendwa wao, Ndugu Hafidh Ameir Hassan. Tunawaombea Mwenyezi Mungu awape nguvu, subira na faraja katika kipindi hiki cha majonzi, na ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi.



