WORLD WATERNET WAKAGUA MIRADI YA UHIFADHI NA UWEZESHAJI JAMII NGERENGERE.

Wadau kutoka Shirika la World Waternet kwa kushirikiana na Wami/Ruvu pamoja na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Moruwasa wamefanya ziara ya kukagua maendeleo ya miradi ya uhifadhi wa mazingira na uwezeshaji jamii inayotekelezwa katika maeneo yanayozunguka Bwawa la Mindu, mkoani Morogoro.
Katika ziara hiyo, wadau wametembelea Kijiji cha Tangeni na kukagua kitalu cha miche ya matunda kinachoendeshwa na wananchi kinacholenga kuongeza kipato cha jamii kupitia uzalishaji na uuzaji wa miche sambamba na kuchangia uhifadhi wa mazingira.
Aidha wamekagua ujenzi wa banio (check dam) katika Mto Ngerengere unaolenga kudhibiti mmomonyoko wa udongo na kupunguza mchanga na tope vinavyoingia katika Bwawa la Mindu.
Wadau pia wametembelea vituo vya ufuatiliaji wa taarifa za maji na hali ya hewa katika eneo la Bwawa la Mindu na kukagua matumizi ya teknolojia katika ukusanyaji wa taarifa muhimu kwa ajili ya usimamizi endelevu wa rasilimali za maji.
Ziara hiyo imeimarisha ushirikiano kati ya Bodi ya Maji Bonde la Wami/Ruvu, World Waternet, Moruwasa, Serikali za Mitaa na jamii katika uhifadhi wa mazingira ulinzi wa vyanzo vya maji na matumizi endelevu ya rasilimali za maji kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho.
Tonelamajilazimalihifadhiwe



