WRBWB imeandaa utabiri wa wingi wa maji katika Mto Ruvu kwa kipindi cha kuanzia tarehe 12 hadi 22 Februari, 2026.

WRBWB imeandaa na kuwasilisha utabiri wa wingi wa maji katika Mto Ruvu kwa kuzingatia vituo vilivopo katika Kidakio kwa kipindi cha kuanzia tarehe 12 hadi 22 Februari, 2026 ambapo utabiri huu umezingatia utabiri wa hali ya mvua na joto zilizotolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA).
Utabiri unaonyesha wingi wa maji utaongezeka na kuwa juu ya wastani wa muda mrefu (2009-2024) kuanzia tarehe 21 Feb,2026 kutokana na uwezekano wa kuwepo na mvua katika safu ya Milima ya Uluguru. Kiwango cha maji kilichopo kwa sasa na siku kumi zijazo ni himilivu na kinatosheleza mahitaji ya sekta mbalimbali ikiwemo mahitaji ya maji majumbani katika Mitambo ya DAWASA ya Ruvu Juu na Ruvu Chini.
Bodi inapenda kuwashauri watumiaji wa maji katika sekta ya Kilimo, Mifugo, Mamlaka na Wakala wa Maji Safi na Usafi wa Mazingira kuchukua tahadhari pia wahakikishe wanakuwa na njia mbadala ya upatikanaji wa maji ikiwemo visima virefu endapo kutatokea upungufu wa maji katika Mto Ruvu.
Bodi itaendelea kutoa taarifa ya mwenendo wa wingi wa maji kila baada ya siku kumi na kuwahabarisha wanufaika na Mto Ruvu ili waendelea kuchukua hatau za tahadhari dhidi ya kupungua kwa wingi wa maji katika Mto Ruvu kwa siku zijazo.
“Tone la maji lazima lihifadhiwe “



