WAMI/RUVU YASHIRIKI MKUTANO WA 7 WA JUKWAA LA TAIFA LA WADAU WA SEKTA MTAMBUKA KATIKA USIMAMIZI WA RASILIMALI ZA MAJI.

WRBWB imeshiriki katika Mkutano wa Saba wa Jukwaa la Taifa la Wadau wa Sekta Mtambuka katika Usimamizi wa Rasilimali za Maji (07th National Multisectoral Forum on Water Resources) lililofanyika mkoani Dodoma kwa lengo la kujadili masuala ya kimkakati yanayohusu usalama wa maji nchini.
Mkutano huu umejadili sera,mikakati na teknolojia bunifu zitakazosaidia kuimarisha usalama wa maji kama nguzo muhimu ya ustawi wa taifa na maendeleo endelevu.
Kupitia Mkutano huu, WRBWB imepata fursa ya kubadilishana uzoefu na wadau mbalimbali wa sekta ya maji, mazingira, nishati, kilimo, viwanda na maendeleo ya kijamii juu ya namna bora ya kusimamia rasilimali za maji kwa kuzingatia misingi ya ustahimilivu, usawa na uendelevu, kama inavyoelekezwa katika Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.
Ushiriki wa WRBWB umejikita katika kuonesha umuhimu wa ushirikiano wa wadau katika kulinda, kuhifadhi na kutumia rasilimali za maji kwa njia endelevu, sambamba na kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya tabianchi, ongezeko la mahitaji ya maji, pamoja na ukuaji wa shughuli za kijamii na kiuchumi.



