WRBWB YASHIRIKI MKUTANO WA 9 WA BODI ZA MAJI ZA MABONDE

Bodi ya Maji Bonde la Wami/Ruvu imeshiriki katika Mkutano 9 wa Mwaka wa Bodi za Maji za Mabonde Nchini (9th Annual General Meeting), uliofanyika tarehe 27 Januari 2026 mkoani Dodoma chini ya uratibu wa Wizara ya Maji, na kukutanisha viongozi wa Sekta ya Maji kwa lengo la kupitia taarifa za utekelezaji wa mipango ya usimamizi wa rasilimali za maji katika Mabonde mbalimbali, kujadili changamoto na mafanikio yaliyopatikana katika utekelezaji wa Programu ya Uendelezaji wa Sekta ya Maji katika kipindi cha mwaka (2021 – 2025).
Akisoma Taarifa ya thamini iliyofanywa na Wizara ya Maji kwenye Mabonde, Mkurugenzi Msaidizi Mipango, Ufuatiliaji na Tathmini Kutoka Wizara ya Maji; Pamella Temu ameitaja WRBWB kushika namba moja kati ya Mabonde 9 ya Maji yaliyopo nchini katika utendaji wa kazi na kuhakikisha usimamizi wa rasilimali za maji unakuwa endelevu.
Mkutano wa 9 wa Bodi za Maji za Mabonde umeonesha dhamira ya serikali na wadau kuhakikisha rasilimali za maji zinasimamiwa kwa ufanisi kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho.
Kaulimbiu ya Mkutano ni “Uhakika wa Maji kwa Maendeleo ya Taifa: Utekelezaji wa Dira 2050 katika Ustahimilivu, Usawa na Uendelevu”.



