WRBWB Yakarabati Vituo vya Kupima Mwenendo na Wingi wa Maji Mitoni.

Bodi ya Maji Bonde la Wami/Ruvu inaendelea na zoezi la ukarabati wa vituo vya kupima mwenendo na wingi wa maji katika Kituo cha Wami Mandera na Wami Dakawa.
Ukarabati wa vituo hivi ni hatua muhimu katika kuhakikisha upatikanaji wa takwimu sahihi za rasilimali za maji, zitakazosaidia katika utoaji wa taarifa sahihi na maamuzi bora ya usimamizi wa Rasilimali za maji.
Bodi inaendelea kuwahamasisha wananchi kuchukua tahadhari kwa kufuatilia taarifa za hali ya hewa kutoka kwa mamlaka husika na kuendelea kutunza rasilimali zetu za maji.



