DIRA 2050
emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Maji
Bodi ya Maji Bonde la Wami/RUVU
ega Logo
Habari
ega-svg-tree

MOROGORO, Julai 2, 2026
Watumishi wa Bodi ya Maji Bonde la Wami/Ruvu wametakiwa kuanza mwaka wa fedha 2026/2027 kwa kuzingatia uwajibikaji, nidhamu ya kazi na matumizi sahihi ya mifumo ya utendaji ili kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu ya taasisi.
Maelekezo hayo yametolewa na Kaimu Mkurugenzi Bi. Janeth Kisoma katika kikao cha watumishi kilichofanyika katika Makao Makuu ya ofisi za Bodi ya Maji Bonde la Wami/Ruvu mkoani Morogoro, ambapo watumishi walikumbushwa wajibu wao wa kutekeleza majukumu kwa weledi, uadilifu na kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za Utumishi wa Umma.
Katika kikao hicho, watumishi walielekezwa kuendelea kutumia Mfumo wa PEPMIS kwa ufanisi katika upangaji, utekelezaji na tathmini ya malengo ya utendaji huku wakihimizwa kuhakikisha malengo wanayojiwekea yanatekelezwa kwa wakati ili kuchangia mafanikio ya taasisi.
Aidha, kikao kilijadili masuala ya upandishaji vyeo (Promotion), nidhamu kwa watumishi, taratibu za mawasiliano wakati wa kuomba ruhusa pamoja na umuhimu wa kuzingatia muda wa kazi kama msingi wa kuongeza tija na uwajibikaji katika utumishi wa umma.
Sambamba na hilo, watumishi walifahamishwa kuwa utoaji wa motisha (Incentive) unategemea kiwango cha utendaji kupitia Mfumo wa PEPMIS pamoja na mahudhurio kazini. Hivyo, walihimizwa kuzingatia mahudhurio, kutekeleza majukumu yao kwa bidii na kushiriki kikamilifu katika kufikia malengo ya taasisi kwa mwaka wa fedha 2026/2027.
Kikao hicho kilihitimishwa kwa kutoa nafasi kwa watumishi kujadiliana na kutoa maoni kuhusu masuala mbalimbali ya kiutumishi, hatua iliyolenga kuimarisha ushirikiano, mawasiliano na utendaji wenye matokeo katika Bodi ya Maji Bonde la Wami/Ruvu.

Mpangilio

slot gacor