emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Maji
Bodi ya Maji Bonde la Wami/RUVU
ega Logo
Habari
ega-svg-tree

Wananchi wa Wilaya ya Kilosa, Mkoani Morogoro wamehimizwa kutunza mazingira na vyanzo vya maji ili kuendelea kukabiliana na athari zinazoweza kusababishwa na mvua kubwa za El Niño zinazotarajiwa kunyesha katika kipindi cha mwezi Oktoba hadi Disemba 2026
Wito huo umetolewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni katika muendelezo wa ziara yake ambapo ametembelea Mto Mkondoa kujionea hatua mbalimbali zilizochukuliwa za ukarabati wa kingo za mto huo ili kuhakikisha mvua hazileti madhara kwa wananchi wa Kilosa.
Waziri Masauni ameridhishwa na jitihada zilizofanywa na Bodi ya Maji Bonde la Wami/Ruvu za kurekebisha tuta la Mto Mkondoa kwenye kipande cha urefu wa mita 250 kilichokuwa kimeharibika, ikiwa ni hatua ya kudhibiti mafuriko kwa wananchi waishio katika Kata ya Kasiki na kulinda miundombinu ya reli ya TRC (MGR na SGR)
Awali akipokea taarifa ya utekeleza wa kazi hiyo kutoka kwa Afisa Kidakio cha Wami, Mhandisi Lusajo Edwin ameeleza kuwa mbali na ukarabati wa tuta hili pia Bodi imefunga vituo vipya vitano (5) na kufanya jumla ya vituo vya kisasa kufikia 50 vinavyotumika kufuatilia kiwango cha maji kwa muda halisi (real-time) uwekaji wa vituo hivyo kwenye Mto Mkondoa unalenga kufuatilia ongezeko la maji katika mito inayochangia ili kutoa tahadhari ya mapema kwa wananchi, pamoja na kuisaidia TRC kufanya maamuzi sahihi ya kiutendaji kwenye usafiri wa MGR na SGR wakati wa dharura

Mpangilio

slot gacor