Huduma hii inamwezesha Mwombaji kupata kibali cha kutumia maji kihalali kwa ajili ya matumizi yafuatayo;
1. KIBALI CHA MATUMIZI YA MAJI
- Matumizi ya nyumbani (binafsi au kikundi)
- matumizi ya shughuli za kibiashara (hotel, lodge, n.k)
- usambazaji wa maji kwenye Jamii (Mamlaka za Maji)
- kukinga na kuhifadhi maji kwenye Bwawa
- Umwagiliaji mdogo mdogo & mkubwa
- Kilimo-Biashara
- Kunyweshea Mifugo
- ufugaji wa Samaki
- matumizi ya Kiwandani
- kufanya usafirishaji wa Vyombo vya majini kwenye maji baridi (Mito na Maziwa)
- Ujenzi (barabara, majengo, reli n.k)
- shughuli za uchimbaji Madini
- uzalishaji wa maji ya kunywa ya chupa
- uzalishaji wa Nishati/Umeme
2. KIBALI CHA KUCHIMBA KISIMA
- Huduma hii inamwezesha Mteja kupata kibali cha kuchimba kisima kirefu
3. KIBALI CHA KUTIRIRISHA MAJITAKA
- yatokanayo na matumizi ya majumbani
- yatokanayo na shughuli za Viwandani
- yatokanayo na shughuli za Kilimo/Umwagiliaji
4. KIBALI CHA KUPITISHA MIUNDOMBINU YA MAJI
- Huduma hii inamwezesha Mtumia maji kupata msaada wa Kiofisi ili kupitisha miundombinu ya maji kwenye maeneo ya Watu wengine




