Kuelekea Wiki ya Maji Dunia, WRBWB Yapanda Miti Pembezoni mwa Mto Mlali.

Kuelekea maadhimisho ya Wiki ya Maji, WRBWB imeshirikiana na kikundi cha Jumuiya ya Watumia Maji Ngerengere Juu-A pamoja na Wananchi kupanda miti 300 aina ya Mikaranga katika chanzo cha Mto Mlali Wilaya ya Mvomero Mkoani Morogoro. Zoezi hilo ni sehemu ya juhudi za kuhifadhi na kulinda vyanzo vya maji ili kuhakikisha upatikanaji endelevu wa rasilimali maji kwa vizazi vya sasa na vijavyo. Sambamba na upandaji hu...







