UCHAGUZI WA WAJUMBE WAPYA NA MAFUNZO YA KUJENGA UWEZO VYAIMARISHA USIMAMIZI WA RASILIMALI ZA MAJI MGETA CHINI.

Bodi ya Maji ya Bonde la Wami/Ruvu kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro imekamilisha zoezi la uchaguzi wa wajumbe wapya wa Jumuiya ya Watumia Maji Mgeta Chini (WUA) pamoja na kuanza mafunzo ya kuwajengea uwezo viongozi hao ili kuboresha usimamizi na uhifadhi wa rasilimali za maji. Uteuzi wa wajumbe umefanyika kupitia Mabaraza ya Maendeleo ya Kata za Bwakila Chini, Mngazi na Kisaki, zinazojumuisha vijiji vya...








