WAMI/RUVU YASHIRIKI ZIARA YA WAZIRI WA MUUNGANO NA MAZINGIRA KUKAGUA USAFI WA MTO NG’OMBE

Bodi ya Maji Bonde la Wami/Ruvu imeshiriki ziara ya kikazi ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Mhandisi Hamad Y. Masauni, kwa lengo la kukagua utekelezaji wa maelekezo ya Mhe. Makamu wa Rais kuhusu usafishaji na uhifadhi wa Mto Ng’ombe, ikiwa ni pamoja na kukabiliana na El Niño. Waziri amekagua eneo lenye urefu wa takribani kilomita tano kuzunguka Daraja la Mto Ng’ombe...







