WADAU WATATHIMINI UTEKELEZAJI WA MRADI WA UHIFADHI BWAWA LA MINDU, WAPANGA MABORESHO YA AWAMU YA PILI.

Bodi ya Maji Bonde la Wami/Ruvu kwa kushirikiana na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Morogoro (MORUWASA), World Waternet na Shirika la Kilimo Endelevu (SAT) imefanya kikao kazi cha kutathmini utekelezaji wa awamu ya kwanza ya Mradi wa Uhifadhi wa Bwawa la Mindu. Kikao hicho kimelenga kupitia maendeleo yaliyofikiwa, kutambua mafanikio yaliyopatikana pamoja na changamoto zilizojitokeza katika utekelezaji wa mradi katika eneo la mf...








